Wewe kama Mwafrika-2c
Mwaka 995 KK, Ethiopia: mfalme Sulemani
na Makeda Bilqis (malkia wa Sheba)
wakuwa na mahusiano na walizaa mtoto wa kiume aliyeitwa Meneleki I, ambaye alianzisha utawala wa kinasaba na wa Mfalme
Sulemani zaidi ya miaka 3000 iliyopita (1000KK) ambapo walikuwa wana tamaduni
za Kiyahudi na mfumo wa utawala wao, historia inatuambia
kuwa Haileselasi ni
Mfalme wa mwisho wa utawala huo ambao ulianguka
Meneleki I |
mwaka 1974, kwa kuingia kwa
falsafa na mawazo ya kishenzi ya kikomunisti kutoka Urusi (Ndiyo, mawazo ya kishenzi).
Historia ina chambua na kuchimba zaidi kuwa Sanduku la Agano lilihifadhiwa na
Meneleki huko Ethiopia na kupelekwa Aksum ambapo makasisi walilitunza. Kwanini
mambo haya yanafichwa na tunadanganywa? Mwaka 500 KK huko
Elephantine, Waisraeli walikaa pembezoni mwa mto Nile katika kisiwa cha
Elephantine Kusini wa Misri. Ambapo walianzisha mkakati wa kijeshi wa kulinda
biashara ya Misri na Nubia.
Baada ya anguko la Yerusalemu Waisraeli hawa
walikwenda na kukimbilia Misri mwaka 586
KK(BC) wakiwa na Yeremia; ambapo baadhi wanaamini kuwa Waisraeli walikuwa
huko mapema zaidi ya hapo (jambo ambalo
ni kweli kabisa, Rejea habari ya Yusufu). Ambapo inaaminika kuwa baadhi
walikuwa ni moja kati ya wana kumi wa kabila; ambao walikuwa wamepotea, ambao
walikuwa wamesafirishwa kwa utumwa mwaka 722
KK kwenda Assryia na baadaye Babilonia na baadaye Misri. Hii ni kwa sababu
mahekalu ya Elephantine yalikuwa yanafafana kwa kiasi kikubwa mno na majengo ya
hekalu la Shiloh yaliyojengwa huko Falme ya kaskazini na hayo makabila
kumi.
Elephantine temple liliharibiwa na Misri mwaka 410KK na hapo ndipo wana wa
Israeili wakasambaratika tena. Huko Aljeria mwaka wa 5 (5AD/BK) wanahistoria kwa
hoja na vielelezo wanasema kuwa Waisraeli walifika huko, “Tamentil” mji wa
Waisraeli ambapo walipanda na kuvuna michikichi na mawese (je huko kwenu kuna mahali kuna michikichi na mawese?) pia walijenga
vijiji. Walikuwa ni watu wenye kumiliki mali, utajiri (rejea Mansa Mussa tajiri mashuhuri duniani) mashujaa na waliishi na
kuwepo hadi mwaka 1437(swali kwani
historia hii ya miaka nyuma ya karne 16 inafichwa linaweza kuibuka), kabla ya
kuvamiwa na Wahamaji (Nomads) Waarabu
ikiwa ni pamoja na kuporwa mali zao. Kulifanyika mauaji makubwa sana mwaka 1492
ambayo yalifanya watu kuzikwa kwenye makaburi mengi, Waarabu waliua karibia
kuwamaliza kabisa. Ushahidi wa makaburi yao uko huko Tuat-Guara.
Mabaki ya Elephantine |
Cyrene, Libya mwaka 125BK Waisraeli
wali kimbia dhidi ya uliokuwa uvamizi wa kidhalimu wa Warumi na kwenda huko
Libya, vita ile ilikuwa maarufu kwa jina la “Roman Jews War”. Kisa ikiwa ni kuanzisha taifa la Kiebrania ila
Warumi waliwafukuza na kuwasogeza huku Arika (Ndio sisi). Wazungu kwa aibu na wizi wa historia hawawezi kukuambia
ukweli wote wa haya na ndio maana wamefanya mbinu kwa masharti ya kuondoa historia
ya mtu mweusi, kwa kupanga mitaala na nchi nyingi za Afrika zikaondoa mitaala
ya Historia kwa ngazi ya msingi (na
historia kubwa tunayosoma ni kuanzia miaka ya 1600, 1800 na sasa). Tunatakiwa kusikia aibu kwa kukataa
historia yetu wenyewe kwa mapokeo ya kiimani!
Ukisoma juu ya habari ya Ghana utaona maajabu na uwezo wetu sisi kama
Waisraeli; mwaka 300BK, “The Za Dynasty”
karibia miaka 200 baada ya kufukuzwa kutoka Yerusalemu baadhi ya Waisraeli
walianza kuanzisha taifa zao huko Yemeni. Ambapo baadaye walihamia Timbuktu
Afrika kwenye kitovu cha ustaarabu wa dunia ya kale. Za el Yemen ilikaliwa na
kuanzishwa na hawa Waisraeli ikiwepo Falme ya kale ya Ghana na hii The Za
Dynasty ambao walikuwa jamaa wa Wafalme wa Israeli. Asikudanganye mtu tena
kwamba hawa wa sasa ni Waisraeli!.
Eneo hili kwa sasa linaitwa Mali, ambapo
watu wake ni miongoni mwa makabila kumi ya Israeli waliopotea mwaka 722KK na
hawa Assyrians (2Wafalme 17:6).na hii
wanazuoni wa biblia wanalifahamu ila hawasemi ukweli wote, wanadonoa na kukaa
kimya. Ukisoma maandiko matakatifu Isaya 52:4 Walikuwa wanafuata sheria za
Mussa (Torah) na wala sio “Talmud”.
Mwaka 600 eneo hili lilitekwa na kutwaliwa na Waislam hapo ndipo kuzaliwa kwa
biashara ya Sahara kupitia Ghana. Biashara ile ilifanya eneo lile kuwa tajiri
sana na kwa mwaka 1000BK Wafalme Waisraeli wa Ghana walibadili dini na kuwa
Waislamu ilikufanya biashara kati yao na wafanyabiashara wa Arabia kuwa nzuri
na rahisi (Walianza kumsahau mungu wao).
Mali ilikuja kuwa “Songhay Empire” wakati wa Sonni Ali ambaye alikuja kuwa Mfalme wa mwisho katika zama za
Wafalme. Mfalme Sonni Ali akuwa mmoja wa Wafalme, japo alibadili dini na kuwa Mwislamu
aliendelea kuwa mtiifu katika sheria za Musa. Ufalme uliisha baada ya miaka
1200 ambapo ilikuwa 1492.
Endelea..
Makazi ya Wayahudi Weusi Mto Nile |
Endelea..
danmachete666@gmail.com
JibuFutanaomba tujadili baadhi ya vitu,,nitafute kwa hio email,,please naomba sana
Kazi nzuri sana naipenda.Naomba muchapishe kazi kuhusiana na kabila za waizraeli zilozopote hapa africa.
JibuFuta