Alhamisi, 31 Agosti 2017

SAFARI ZA KUHAMA KWA wAISRAEI WEUSI WALIOPOTEA

Tanzania Conservatives     Agosti 31, 2017     No comments


Upande wa Kusini wa Afrika inajulikana kwa jina maarufu kama Afrika ya Juu. Ukisoma kwenye maandiko na vitabu mbalimbali vya kihistoria wanasema juu ya Misri ya Juu na Misri ya chini. Niweke wazi kuwa ukisoma au kusikia Misri yaa Juu tambua kuwa ni Misri ya Kusini na ukisikia au kusoma Misri ya Chini tambua kuwa ni Misri ya Kaskazini. Hii inatokana na jografia ya bara la Afrika. Naweza kusema kuwa moja kati ya mijongeo wa kutoka Kusini kwenda Kaskazini wa miaka ya hivi karibuni ni ule uliofanywa na Waethiopia miaka ya 1990 baada ya uliokuwa uvamizi wa Warusi nchini humo wa kumtoa utawala wa Kiebrania uliofanyika miaka ya 1960, ambapo kundi wa watu

jamii ya Falashas walitoka Ethiopia kwenda Israeli katika ilikuwa inaitwa “Operation Moses”, mjongeo huo haukuhusisha kundi kubwa la watu. Kwa kuangalia historia Wakushi waliokuwa wanakaa Kusini mwa Misri walipanda kwenda Kaskazini na kuweza kuivamia iliyokuwa Misri ya kale na kuitawala. Japo tamaduni za KiMisri ziliendelea kutokana na kuwa watu wa jamii moja na walielewana hata kwa lugha. Jamii hii ya Wakushi waliacha marejeo mbalimbali ya kihistoria japo kwa kiwango kikubwa yameangamizwa (nitafuatilia juu ya hili huko mbeleni). Ukiangalia mwenendo wa Wangoni kutoka iliyokuwa ngome ya Wanguni kuja, Msumbiji, Zambia, Malawi Kusini mwa Tanganyika katika mkoa wa Ruvuma na kwingineko, ni moja kati ya mgawanyiko wa jamii hiyo. Wangoni wanasifika kwa mbinu zao za kivita na pia shughuli mbalimbali, ila swali la msingi hapa ni kwa nini walishindwa katika mapigano katika ngome yao ya kale?


Wangoni au Wanguni ni moja kati ya watu wa jamii ya Wabantu na hawa wanaongea lugha inayoitwa Kinguni au Kingoni ambacho kimetawala kwa kiasi huko Kusini mwa Afrika. Jamii hii inajumuishwa watu wa kabil za Xhosa, Wazulu, Ndebele na Waswazi ambao wanaishi huko Swaziland na Afrika Kusini. Watu jaamii ya Wandebele wanaishi maeneo ya Zimbambwe. Baada ya kugawanyika kutoka Sotho-Tswana na Tsonga, Wangoni walikutana na wawindaji wa San jambo ambalo linaeleza juu ya sauti yao kama lugha ya “kugonga”. Wapo pia Wangoni waliokwenda kuishi huko Kusini Magharibi kwa miaka ile na kujichanganya na Waxhosa na wale waliokwenda kuishi Kusini Mashariki walibaki kujiita Wangoni/Wanguni. Kuibuka kwa Ngome ya Zulu mwaka 1815-1840, kulifanya mataifa/ makaabila mengi yaliyokuwa yameungana kuanza kusambaratika. Hapo ni hadi pale ambapo Mpiganaji na kiongozi wa Wazulu Shaka alipowashinda Wandwande ambao walikimbia kutoka Kusini Mashariki na kwenda kuelekea Kaskazini jambo ambalo lilifanya kubaki kwa kabila za Wazulu na Waswazi. Baada ya kushindwa katika mapigano Zwide na Wandwandwe; makomando wake wawili Shoshangane na Zwengendaba waliwachukua watu wao na kuelekea Kaskazini zaidi na kuenea zaidi kila wanakoelekea. Bwana Shoshangane aliweza kuanzisha utawala wake wa Shangane huko Msumbiji na Zwengendaba alikwenda Tanganyika. (Swali la kujiuliza, je Tanganyika iliundwa na akina Zwengendaba?). Zwengendaba alikuwa akitumia mbinu kama za Wazulu katika mapigano yake. Alikuwa akiwapiga mahasimu wake kisha kuwaunga na kabila lake.


Kifo cha Zwengendaba miaka ya 1840 kilipelekea kurudi nyuma kwa kuanzishwa kwa taifaa la Wangoni, ambapo  wengi walirudi nyuma kulikuwa na mgawanyiko wa makundi matano. Makundi matatu kati ya haayo yalirudi huko Malawi na kuanzisha Ufalme wao na hao wengine; makundi mawili Watuta na Wagwangara walisogea kaskazini zaidi kuingia Tanganyika. Hawa Watuta walienda kaskazini zaidi ambapo moja ya kundi lao liliweza kujichanganya na Wanyamwezi huko ziwa Viktoria na kisha kuweza kukaa huko magharibi mwa Kahama. Miaka ya 1858 Wangoni walishindwa huko Ujiji maeneo ya ziwa Tanganyika na waliokuwa wauza na watekaji wa watumwa. Pia Machifu wa Kinyamwezi walijizatiti kijeshi dhidi ya waporaji na wavamizi wa kingoni. Wakati huo huo Wagwangara walijikita naa kuendeelea huko kusini masharriki mwa Tanganyika na kuunda Ufalme mbili tofauti ambazo ni Njelu na Mshope. Hapa walikuta pia waliokuwa wanaongea lugha jamii ya kinguni kutoka Afrika kusini, Wamaseko. Wakati Wangoni wa Zwengendaba wakielekea huko Malawi hawa Wamaseko walihama kuelekea Msumbiji na kuiga baadhi ya tamaduni za watu wa jamii za hapo na kisha kuvuka Mto Ruvuma miaka ya 1840 na kisha kufika Songea. Huko walianzisha maakundi kama ndonde, Nindi, Ndendeuli, an kisha kuwaunga na Njelu na Mshope.


Mzilikazi katika kukimbia kwake kutoka kwa Shaka aliua wanaume wa eneo husika na kuchukua wanawake na kuanzisha taifa lake jipya lililoitwa Matabele. (Kwanini Mzilikazi alikuwa anamkimbia Shaka?) Mwanzoni kabisa alikaa huko kunakoitwa sasa Pretoria kisha kwenda Mosega karibu na huko Zeerust, baada ya kupigwa na Voortrekkers alikwenda Zimbabwe na kuanzisha mji wake ulioiwa Bulawayo. Kisa cha Mzilikazi kumkimbia Shaka kilikuwa kama ifuatavyo; Mzilikazi alikuwa mmoja wa majenerali wa Shaka Zulu alikuwa Mkhumalo. Wakati aliporudi kwenye mapigano alirudi naa ng’ombe wengi aliofanikiwa kupora na kuiba hivyo akajiwekea kama mali zake badala ya kupeleka ng’ombe kwa Shaka. Hili lilikuwa kosa kubwa na adhabu yake kuwa kali hadi kufa, hivyo akakimbia kutoka ardhi ya Zulu na kwenda kwenye ngome dhaifu za Manala Ndebele.

0 maoni :

Popular Post

Subscribe to Newsletter

We'll never share your Email address.
© 2015 Tanzania Conservative. Designed by Conservative. Powered by Blogger.