Alhamisi, 3 Agosti 2017

JE WEWE NI NANI?-3

Tanzania Conservatives     Agosti 03, 2017     1 comment

D

Hila na dhuluma dhidi ya mtu mweusi-3a

Jambo kubwa lililofanyika na Warumi ni kufuta makumbusho ya kihistoria ya mtu mweusi, mfano iliyokuwa ngome ya Chifu Mkwawa wa Wahehe ambaye alikuwa na asili ya Kiisraeli, msomi wa kubobea shujaa wa Afrika aliyekuwa na lengo kubwa la kujenga utawala mkubwa kama ule wa Kongo na Zimbabwe huko kusini akiangalia historia ya Kilwa na ndoto kubwa ya kurudisha Ufalme ule kwa njia mpya (pengine ndio Tanganyika). Ngome ya Mkwawa ilivunjwa kabisa na masalia yake yakatokomezwa kabisa vito na vitu vya kihistoria pale vikaibwa; historia inatuambia kuwa ngome ile ilikuwa ikipigwa mabomu kwa siku nne mfululizo. Kuna nadhari zinasema kwa Chifu Mkwawa hakuwa amejiua, alifanikiwa kutoroka na alienda kuishi maisha ya kawaida kwa kujificha dhidi ya Wajerumani.
Swali la kujiuliza ni kwa nini Wajerumani walikuja na kichwa ambacho kimeungua wakidai ni yeye huku mwili haujulikani ulipo?

Mmoja wa Farao
Historia ya Ethiopia ya mwaka 955 KK imefutwa kabisa na kuvurugwa makusudi ilikuchanganya mfuatiaji, utagundua kuwa baadhi ya wanahistoria wanadai kuwa Ethiopia ilikuwa eneo ambalo kwa sasa ni Yemen na pia wanadai kuwa Babeli ilikuwa huko. Huku wakifanya tafsiri zisizosahihi za Biblia juu ya mfalme Sulemani na malkia wa Sheba (Makeda Balqis) kwamba hawa kuwa watu weusi. Jambo hili wanahistoria na wanazuoni wa biblia wanafahamu wazi kwamba mtoto wa Makeda yaani Meneleki I ndiye aliyekabidhiwa sanduku la agano na kulihifadhi huko Ethiopia katika milima chini ya Walawi wa kweli. kwa nini kufanya njama juu ya ukweli huu? Mwaka 1964 warusi walifanya hila ya kumtoa mfalme Haile Selassie madarakani ilikuua nguvu ya kisiasa ya Wayahudi duniani (nikisema Wayahudi na maanisha mtu mweusi si hawa wa leo). Unaweza kukumbuka nguvu ya kisiasa ambayo ilikuwepo miaka ile ya 1960-1984 kabla ya kuondoka madarakani kwa Mwl Nyerere, na ndoto kubwa ya kufanya Afrika kuwa nchi moja. Ni ndoto zile za kutaka kuinua upya utawala na taifa la kale la Israeli. Amini ninachokiandika, kuwa siku Waafrika wakitambua historia yao halisi ni siku ambayo dunia hii itarudi kuwa mpya na yenye amani.

Ukweli juu ya Mafarao wa Misri ya kale unapotoshwa kwa kuchora michoro mipya au kupaka rangi mpya michoro ya zamani kuonesha kuwa walikuwa ni watu weupe. Ukiangalia katika maandiko cheo cha Farao kilikuwa kinatolewa kwa kurithisha kizazi kimoja hadi kizazi kingine iweje wawe hao wanao dhaniwa sasa. Rejea juu ya wana wa Ham (Baba Wa Misri, Libya, Ethiopia Na Kanani) ambaye ni baba wa mtu mweusi kwa mujibu wa maandiko.

Namer & Hor- Aha hawa walikuwa Mafarao wa kwanza kwa mujibu wa wanahistoria ambapo Misri ya Kusini na Kaskazini zililetwa pamoja mwaka 3015 KK na Farao huyu aliaminika kuwa na nguvu kubwa ya kupambana na adui zake ushahidi wa hili una patikana kando ya mto nile huko kunakoitwa Hierakonapollis ambapo kulipatikana vito na mapambo meusi iliyopatikana miaka hiyo kabla ya
Piramidi la Farao Djoser
Kristo. Ambaye inaeleza kuwa Farao huyu alikuwa wa kutokea Misri ya Juu. Hila hapa ni kupaka rangi mpya michoro ilikupoteza ushahidi wa watawala halisi wa iliyokuwa Misri. Kwanini maigizo ya kuhusu Misri yanaonesha mtu mweupe ilihali kwenye piramidi ni watu weusi? Prof. David O’Connor anaeleza kuwa Farao ni kiongozi ambaye hana utawala wenye ukiritimba na hii iliweza kusaidia kuwezesha upatikanaji wa kile ambacho kina takiwa kupatikana kwa wakati husika. Na anasisitiza kuwa ni vyema kukumbuka kuwa karibia asilimia 5% ya Wamisri wote ndio waliokuwa wana elimu ya wakati huo. Pengine ndio sababu ya kusaulika kwa maana ya maneno ya kwenye piramidi na historia yake. Ujinga bado unazidi kutumaliza hapa ndio inaingia hila ya kumdumaza Mwafrika kuweka mfumo wenye ukiritimba na urasimu mkubwa na kunyima kizazi chake elimu bora! 

Farao aliyeitwa Djoser (2630 KK) ambaye alikuwa mwendelezaji mkubwa wa taaluma mpya ya ujenzi kwa kutumia mawe huko Saqqara na ndiye Farao aliyejenga piramidi la kwanza kabisa Piramidi la Djoser (kwa jina lake). Japo historia haiweki sawa na wazi juu ya utawala wake ila inaonekana kwamba utawala wake ulitanguliwa na Pharaoh Nebka, ambapo kwa kuangalia sifa za kofia za mafarao, inaonekana kama vile Farao Djoser
Farao Djoser
aligawiwa madaraka kutoka kwa Farao wa Misri ya kusini (Misri ya juu) jambo hili historia haielezi sawa sawa. Mji ulikuwa upo kusini mwa mji huu wa Cairo ya sasa, ulikuwa umejengwa kwa mawe na nguzo imara kupata kuwahi kujengwa leo hii. Utawala wake ulikuwa umeenea karibia Misri nzima kutokana na miongozo yake. Ndiye ambaye alianza usafirishaji wa vito vya thamani huku Sinai Peninsula. Aliendelea kutanua utawala wake huko Abydos, Thebes na Aswan, kudhihirisha nguvu ya utawala wake Djoser alijenga kwa mara ya kwanza katika historia Piramidi. Prof. David Silverman wa Chuo kikuu cha Pennyslevania anasema kuwa Mfalme Djoser ni mtu wa kwanza katika historia ya dunia kujenga jengo kwa kutumia mawe. Jambo kubwa ambalo Farao Djoser anaweza kukumbwa leo hii baada ya kifo chake mwaka 2649KK ni ujenzi wa piramidi kubwa la kwanza linaloonekana hadi leo hii (hapakuwa na watumwa)

1
replies

Popular Post

Subscribe to Newsletter

We'll never share your Email address.
© 2015 Tanzania Conservative. Designed by Conservative. Powered by Blogger.