Hila na dhuluma dhidi ya mtu mweusi-3b
W.E.B. Du Bois (1915), “The
Negroes” anaandika na kusema kuwa Wabantu (Nilotic Negroes) walifanikiwa
kupigana na kuwasukuma “Bushmen” au Hottentot (type of Negores) huko Kusini na
Magharibi mwa Afrika kutoka eneo la maziwa makuu (Afrika Mashariki na Kongo) anasema
kuwa Negroes walikuwa huko Ufa wa Nile (Nile
valley) ambapo uzao wa pili ulichanganyika
na kuwa na damu ya Semetic (Waebrania, Wayahudi au Waisraeli) anadai
kuwa kwa miaka zaidi ya 5000 KK, machotara (mulatto) wa Kimisri na Wazungu
walikuwepo na walikuwa wakiishi huko Bonde la Mto Nile kwenye maporomoko ya
kwanza, na Negroes walikuwa wakiishi kwenye maporomoko ya pili ambao anadai
kuwa damu ya Uisraeli (semitic blood) ilikuwa imechanganyika zaidi
au kidogo.
Anasema kuwa jamii hii ndiyo sasa ni wazawa wa Somali, Gala, Bishari, na Beja
za sasa na kusambaza damu hii huku Red Sea na Uarabuni. Anasema kuwa biashara
na kuhamahama kunaifanya historia ya Wabantu wa Maziwa Makuu kuwa ngumu
kuelezeka na kuielewa. Anasema kuwa kuna
unasibu mkubwa mitatu, kwanza ni kwamba asili ya Wabantu wa maziwa makuu ni
Misri,kama waamiaji wakutokea Kaskazini mwa utawala wa mwanzo wa Misri waliokuja
kushika na kutawala soko la kusini ya Misri, pili ni Waebrania, Wayahudi,
Waisraeli (Semitic) waliokuwa
wameathiriwa na Uarabu na Uajemi; tatu, ni Wabantu (yeye amesema Negros) kutoka
Magharibi na Afika ya Kati, (Bois, (1915), The Negroes, uk. 97).
Moja ya majengo ya Kilwa |
Upatikanaji wa teknolojia kati ya Wabantu katika kilimo cha umwagiliaji, uchimbaji
wa madini, ufugaji uliwasaidia kuweza kufanya biashara sehemu mbalimbali duniani.
Wabantu walifanya biashara hadi Asia ya mbali. Biashara ya Dhahabu, kopa na
silva iliwapa nguvu na inasemekana pia ndio moja ya dhahabu zilizokuwepo huko Ophir. Jambo hili lilifanya kujengwa kwa
taifa huko Benomotapa, Zimbambwe ya sasa. Ambapo kuta zake imegundulika kuwa
zilikuwa zimejengwa kwa ustadi mkubwa sana . Jengo lilikuwa ni ngome iliyokuwa
na sehemu ya kuweka wanyama, karakana, sehemu za kulala, na uwanja kubwa. Kuna masalia
mbalimbali ya kale yaliyopatikana huko Zambezi na maeneo mengine, sanaa ambazo
ni nzuri za kuvutia.
Mwaka 1590, huko ambako kwa sasa ni nchi ya Msumbiji kulikuwa na usambaaji
mkubwa watu usiokuwa na idadi wakitokea huko Mwanamutapa (Monomotapa) hawakuacha kitu chochota kusalia. Bois katika kitabu chake aliwaita hawa wapagani. Imeelezwa juu ya
ujio wa watu waliokuwa wanaitwa Zimbas;
watu wanaotisha ambao hawajawahi kuonekana waliokimbia nchi yao huko na kuja
waliokuwa wamepita sehemu kubwa ya Ethiopia wakiwa wanaua kila kitu kilichopo,
kama ambavyo miaka mia nne Wazulu walivyojipanga. Mwaka 1602 watu kutokea ndani
kabisa, waliokuwa wanaitwa Cabires/Canibbals
“Wala watu” waliingia kwenye Ufalme wa Mwanamutapa, na Mfalme aliyekuwa
anatawala pale alikuwa dhaifu na ufalme wake ukaanguka na kutawanyika mpaka
sasa kuwepo kwa Kaffir-Zulu.
Mwandishi wa Kiarabu aliyeita Macuodi, alifika
iliyoitwa Bahari ya Hindi kwatika Afrika a mashariki na kukuta vitu vyenye
asili ya Uarabuni ila hakukuta makazi yoyote yaa Waarabu isipokuwa wakazi wa
huko waliitwa Wabantu au kama wanavyojiita wenyewe Wazenji, wakiwa wametwaa
nchi kusini mwa Sofala na walikuwa wamepakana na Bushmen (Bushmen ni wakina
nani hasa?) kiongozi wao alikuwa ana cheo kinachoitwa “Waklimi”( The Negros,
pg. 50). Na nchi hiyo ilikuwa ikizalisha dhahabu kwa wingi sana huku ngozi ya
Chui ikitumika kama vazi. Mwaka 1330 Ibn Batuta alikwenda Kilwa ambayo ilikuwa
kiungo kizurisana cha kibiashara Afrika mashariki ambapo Kilwa yenyewe ilikuwa
na misikiti zaidi ya 300, Batuta alijizolea ushindi dhidi ya Wazenji/Wabantu. Baada
ya kutekwa kwa Kilwa, Sofala ilisimama kutokea Mogadishu. Hata hivyo Kilwa
ilikuwa kama kitovu kikuu cha taifa zingine ikiwemo Zanzibar, Msumbiji, na
mamlaka zingine (Tanganyika haijatajwa kwa jina!, kwa nini?) Wakati wa utawala
wa aliyekuwa Mfalme wa 43 wa Kilwa baada ya kuutwaa mji, aliyeitwa Abraham
alikuwa akifanya biashara na Watu wa mamlaka ya bara ambao walikuwa mjumuiko wa
kabila nyingi walioitwa Wabantu.
Endelea...
0 maoni :