Ijumaa, 28 Julai 2017

Uhafidhina ni nini?-1

Tanzania Conservatives     Julai 28, 2017     5 comments



 Uhafidhina 

Ni falsafa ya kisiasa inayolenga kulinda, kusimamia na kufuata mila, desturi na taratibu za jamii au taifa fulani. Siasa za kihafidhina zinalenga hasa kujenga utaifa kwa kufuata sheria, tamaduni na katiba ya taifa. Masuala kama kukemea ubadhirifu, ufisadi, uonevu, unyanyasaji uvunjaji wa sheria na katiba ni moja kati ya shughuli zao. Kwa kingereza wahafidhina wanaitwa “conservatives” na uhafidhina unaitwa “conservatism” au “conservativism”. Kwa Tanzania CHADEMA ndio chama kinachofuata falsafa hii, ndio maana unaona wanavyopigana kulinda na kutetea haki za Wananchi.




Baadhi ya Upotoshaji uliopo Tanzania juu ya Uhafidhina:




  1. Mwaka 2013 tarehe 20 Novemba gazeti la MWANANCHI lilipata kuandika makala yenye kichwa cha habari, “Mgombea binafsi mwisho wa uhafidhina”. Nadhani mwandishi walishindwa kupata neno linalofaa. Mwandishi pasi kuangalia maana nzima ya neno “uhafidhina” amejikita katika kueleza mabadiliko ya katiba ya Zanzibar, ufutwaji wa vyama vingi mwaka 1964 kisha kurudi mwaka 1992. Kwa ufafanuzi ni kwamba wahafidhina ndio hao wanaolilia hilo jambo la mgombea binafsi kwa kuzingatia dhana ya kuwepo kwa haki hiyo huko nyuma. Pia ndio waliopigania kurudi kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.
  2. Tarehe 30/11/2015 katika mtandao wa Mzalendo, waliandika makala yenye  kichwa cha habari, “Tuendelee kufaidi matunda ya Uhafidhina”. Mada hii unaweza kuona kwamba inaeleza mema yatokanayo kwayo, la hasha! Mwandishi anaanza kwa kuandika, “Haikushangaza tokea awali kuwa uhafidhina unalindwa,....” akiwa ana maana ya kwamba siasa za upinzani hasa CHADEMA zilikuwa zinalindwa!.  Mwandishi anajianika kwa kueleza kuwa Zanzibar iendelee kufaidi matunda ya uhafidhina, ambapo kimtazamo uchaguzi ule ulikuwa na elementi za siasa za kihafidhina kwa upande wa CUF chini ya UKAWA. Kwa kifupi mwandishi hajui au anajua maana ya uhafidhina ila amejikita kupotosha watu.
  3. Tarehe 12/6/2014, Issa Michuzi katika blogu yake kupitia mwandishi Maalum wa NY, aliandika chapisho lenye kichwa cha habari, “Tuwaepuke vijana wetu na Uhafidhina - Naibu waziri Silima”. Hii ikiwa ni kumnukuu aliyekuwa naibu waziri wa nishati Mh Silima. Katika andiko hilo alifananisha uhafidhina na matukio ya kigaidi yanayoendelea duniani kwa mwaka ule. Ambapo alitafsiri vibaya maneno ya Mh Silima kwamba, “kaika nchi nyingi za Afrika ongezeko la idadi kubwa ya vijana wasio na ajira kunatoa mwanya mkubwa kwao kurubuniwa na makundi yenye itikadi kali”. Mwandishi Maalum ni mnafiki! Vyema kunyambua kuwa kuna hatari kubwa kweli juu ya vijana kukosa ajira ila si kusema kuwa Uhafidhina ni hatari, Hell no!


Elimu


Katika andiko la Mwanakijiji, Jamii Forums aliandika chapisho lenye kichwa cha habari “Uhafidhina ni nini hasa? Maana yake inapotoshwa...” akiwa haja toa majibu ya swali lake la msingi ila aligusia mambo mbalimbali ikiwemo kuzungumzwa kwa neno hilo wakati wa sakata ndani ya CHADEMA mwaka 2013. Maswali yake katika andiko lake yamebakia kuwa wazi hadi sasa ni napo anza kutoa maoni yangu na kueleza nini hasa maana ya Uhafidhina na Wahafidhina.

Itaendelea sehemu ya pili...

5
replies
  1. Kusema kweli Mimi mwenyewe nilikuwa sijui maana ya hili neno 'uhafidhina'ila nimeweza kulitambua baada ya kumsoma mtu aitwae 'Magrat' ambaye alikuwa kiongozi wa chama cha 'conservative party' huko UK na hapo ndipo nilipopata swali nakujiuliza hivi hili neno 'conservative' linamaana gani hasa? Hivyo nikaingia mtandaoni ndio nikapata ufafanuzi mzuri hivyo sasa nimelielewa vizuri sana

    JibuFuta
  2. Kusema kweli Mimi mwenyewe nilikuwa sijui maana ya hili neno 'uhafidhina'ila nimeweza kulitambua baada ya kumsoma mtu aitwae 'Magrat' ambaye alikuwa kiongozi wa chama cha 'conservative party' huko UK na hapo ndipo nilipopata swali nakujiuliza hivi hili neno 'conservative' linamaana gani hasa? Hivyo nikaingia mtandaoni ndio nikapata ufafanuzi mzuri hivyo sasa nimelielewa vizuri sana

    JibuFuta
  3. Uongo chadema siyo wahafidhana mbona wanapinga kiswahili

    JibuFuta

Popular Post

Subscribe to Newsletter

We'll never share your Email address.
© 2015 Tanzania Conservative. Designed by Conservative. Powered by Blogger.