Wewe kama mwafrika-2b
Ukisoma Katika bibia takatifu utagundua kuwa ilifahamika toka mwanzo juu ya fitina na kutolewa wasia wakutokukubali kudanganywa na watu wakidai kuwa wao ndio yeye (Luka 21:8-9). Rejea juu ya habari ya Cesare Borgia aliyekuwa mwanasiasa mashughuri wa Roma miaka ya 1475-1507. Ambapo kuna tetesi kuwa picha ya sasa ya Yesu ilitokana na sura yake, Dumas, “Celebrated crimes (The Borgias)”, vol 1.Cesare Borgia |
Mnamo tarehe 2/7/1706, (hutaambiwa na kanisa
Katoliki juu ya hili) huko Kongo, Katika utawala wa Mbaza binti wa miaka 22 alizikwa
akiwa hai kwa mapinduzi dhidi ya biashara ya utumwa jina lake alikuwa anaitwa Kimpa
Vita. Alikuwa mwanamke shupavu na jasiri; husanisha na maandiko (Yeremia
5:25-26) wakati wa kuwateka Wayahudi weusi kuwa watumwa huko Kongo na
sehemu zote za Afrika walikokuwepo. ikiwa ni ajenda ya kuwaadhibu Misri na Yuda
(Sira 33:15). Athabu kwa wote waliotahiriwa na wasio tahiriwa wote ambao
wamepitia Katika mapito (wilderness).
Soma andiko hili Yeremia 9:25-26, “tazama siku
zinakuja, asema Bwana nitakapo waadhibu wote waliotahiriwa katika hali yao ya
kutokutahiriwa; Misri na Yuda na Edomu na wana wa Amoni na Moabu na wote wenye kunyoa
denge, wakaao nyikani; maana mataifa hayo yoe hayana tohara, wala nyumba yote
ya Israeli hawakutahiriwa mioyo yao”. Unaweza jiuliza swali la haraka
kwanini jina “Tanganyika”? je
linaendana na watu walio itwa wakaao nyikani? Hakika hao ndio. Kumbuka wana hao
wote waliotaja hapo ni wana wa Ham ambaye ni baba wa watu weusi. Endelea kusoma
Ezekia 30:26, “nami nitawatawanya Wamisri kati ya mataifa
nakuwatapanya kati ya nchi mbalimbali; nao watajua yakuwa mimi ndimi BWANA”.
Wanazuoni wa biblia wanajua kwa hoja kuwa Misri ni Waebrania ambao ni watu
weusi wana wa Ham; pia jamii inayozungumzwa hapa ni Waisraeli ambao ni Waafrika.
Prof Louis Losley Marselin mtaalamu
wa Arts anaeleza kuwa waafrika wana aina nyingi ya Sanaa akitolea aina tofauti
ya musiki ambapo ni asili pia ya wana wa Israeli, ikiwa ni pamoja na siri ya
muingiliano wa lugha za Kibantu. Swali kwanini hadi sasa Kongo mambo si shwari?
Na kwanini Wazungu bado wapo hapo? (Zekaria 1:21) ndio jibu. Ambapo Kongo Bena Yahounde wanasadikiwa kuwa ni wayahudi (Judah)
ambao wametokea Katika Jamhuri ya Dominika. Neno Yahounde ni sawa na neno Jews.
Nao wanaamini kuwa Roho wa Bwana ndiye aliyewapatia ala mbalimbali za muziki(Wakongo
ni mashughuli sana kwa muziki) pitia (Sefania
3:10-11). Nchi iliyo mbali na mito ya Kushi ni Kongo unga na rwanda na burundi
ya leo.
Ukisoma Abbe
Proyart, “History of Loango, Kakongo and N’goyo” 1776, (uk. 592-593)
waliandika Wabantu ndio wanandugu na Negros kwa Afrika, ikisema Wakongo
waliondoka Israeli na lugha yao bado inaa maneno ya Kiebrania, Kigiriki na
Kilatini (John 19:20).
Najua kwamba hadi hapa utakuwa tayari
unamejiuliza, “kwanini tunachukiwa hivi?” soma (Ezekia 35:5). Ukisoma Obadia 1:10-11, laana ya Waafrika kuwauza
Waafrika wenzao kama watumwa nakukatwa kwa viungo kwa ndugu hao. Mfalme Leopold
wa Ufaransa ndiye anayeongoza kwa kuua watu wengi duniani na alikuwa akiitawala
Kongo, aliiua Zaidi ya 10 milioni ya Waisraeli(Wakongo). What a shame Europeans! Ambaye alisema kuwa watu wake hao wataitwa
kwa “jina lake” KONGO (H2289), THE BELT, ukweli upo kwenye (2 M Nyakati 7:14), “ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu
watajinyenyekesha, na kuomba na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya;
basi nitasikia kutoka mbinguni, nakuwasamehe dhambi yao na kuiponya nchi yao”.
Sio kwa jina la Mfalme huyo. Nasema tena, “Shame
on you!”
Endelea..
0 maoni :