Jumatano, 2 Agosti 2017

JE WEWE NI NANI?-2d

Tanzania Conservatives     Agosti 02, 2017     No comments

Wewe kama Mwafrika-2d



Warada (Radanites) mwaka 1850, hawa walikuwa Waisraeli ambao alikuwa wakifanya biashara duniani kote na mwishoni kukaa magharibi mwa Afrika, huko Timbuktu. Na hawa Warada ni watu weusi kabisa, na kuna mbinu za kufanya upotoshaji na wengine wanawaita Waarabu weusi, jambo aambalo ni uongo mkubwa na wanazuoni wanajua kwa hoja kuwa wale ni Waisraeli. Watu wa Ghana na Ivory Coast (Ashanti Isralites) ni watu wa iliyokuwa “Ashanti Empire”, ambapo watu wa Ashanti
walikuwa wakutokea huko Mji wa Ashan au Asante kama inavyofahamika na wengine.
Binti waki Falashas

Kuna jamii ya wa Ethiopia inaitwa “Falashas” ambao waligundulika na Wazungu mwaka 1848 wakiwa wako kwa idadi ya watu 45000, wakihusika kuwa na mjumuiko wa Judah, Dan, Naphtali, Simeon na Benjamini wakiishi Torati. Kwanini historia inafichwa, kwanini tunadanganywa, kwanini tunaambiwa tusichimbue sana, kwanini tunatishwa kuwa ni dhambi kujadili masuala ya kidini, mbona “kwanini” ni nyingi sana? Hadi mnamo Mwaka 1930 Ethiopia lilikuwa taifa la mwisho Afrika kuwa huru mengine yote yalikuwa tayari yametawaliwa; mwaka 1938 Ethiopia ilipigwa na Italia (Warumi) lakini baadaye USA walirudisha tena utawala wa Haile Selassie wakati wa vita ya Baridi mwaka (1948-1980) kwa kujenga kituo cha makombora. Baada ya marekani kujitoa  huko miaka ya 1960, Wakomunisti waliwatoa Waebrania nje ya utawala. Aibu gani hii?.. mwaka 1990s kulikuwa na vuguvugu lililokuwa likiitwa “Operation Moses” ambapo walisafirishwa baadhi ya Falashas kwenda Israeli. Walienda kufanya nini? Ni swali kati yangu mimi na wewe.
Mwanaume wa Radanites

Ukisoma Yer. 24:8-9, “Na habari za tini zile mbovu, zisizoweza kuliwa kwa kuwa ni mbovu sana; hakika asema BWANA, ndivyo nitakavyomtoa Sedekia mfalme wa Yuda, na wakuu wake, na mabaki ya Yerusalemu, waliosalia katika nchi hii, na hao wanaokaa katika nchi ya Misri. Naam, nitawatoa watupwe huko na huko katika falme zote za dunia, wapate mabaya; wawe kitu cha kulaumiwa, na mithali na dhihaka na laana, katika mahali pote nitakapowafukuza.” Utajiuliza kwamba, “kwanini Mungu ana hasira kali mno na sisi?”. Hadi hapa wanazuoni wa biblia wanajua wazi kuwa anayezungumzwa ni mtu mweusi na wanajua wazi kuwa Babilonia (Sheshaki) ilikuwa ya mtu mweusi chini ya Nebkadreza ambaye Mungu mwenye anamuita mtumishi wake (Yer. 25:9) hapa ni kweli kwamba Babeli ilikuwa ya Waisraeli, na hao walikuwa ni ndugu mmoja. Hili jambo wanazuoni wanalijua kwa hoja na vielelezo kabisa.

Inaelezwa kuwa Waisraeli wapatao 600 milioni walifanywa watumwa huku
Balozi wa Ashanti, akiwa na Mkufu wa Kabila 12 za Israeli
Afrika na hao waliopelekwa huko Marekani na Caribbean ni miongoni mwao tu. Asilimia 5% walipelekwa Amerika ya kaskazini (Negroes). Ikumbukwe kwamba wengi wa waliokuwa wanawamiliki watumwa ni Wazungu wanaojiita “Jews” na Masons na hawa walipenda kuwachukua watumwa hawa wa Waisraeli wa Kiebrania (Negroes/Africans) kutokana na kujua laana ambayo iko kwenye maandiko matakatifu, (Swali la Waafrika kuwauza Waafrika wenzao linapata jibu, japo wote ni Waisraeli). Biashara ya utumwa imetimiza liliokuwa utabiri wa zaidi ya miaka 3,300 iliyopita (Kumbukumbu la Torati 28:1-68), Kum. 28:15-68, nakusihi sana usome hili andiko kisha usome mema aliyosema pia kuanzia Kum. 28:1-14. Kitendo cha Waafrika kuwauza Waafrika wenzao ni sawa na kuuza nafsi zao, kitendo cha Waafrika kutokufuata maandiko (Torati) ni sawa na kuuza nafsi zao (Kum. 28:68). Kwanini baadhi ya Wakatoliki wanapinga uamsho? Kwanini katika Mtaguso wa Vatikani makadinali karibia wote isipokuwa mmoja walipinga kuwepo kwa uamsho? Kwanini kuna uamsho katoliki? Je Roho wa bwana anapaagiwa namna ya kumtokea mtu? Kwanini uamsho umevamiwa? Kwanini Wasabato hawaamini juu ya Uamsho? Kwanini viongozi wa dini ya Kiislamu watokee kwa familia ya mtume? Kwanini machafuko nchi zenye Uislamu? Kwanini nchi za Kiislamu hawaangalii sana elimu ya dunia? Kwanini Waarabu waliwaua Waafrika katika nchi zao? Kwanini wengi wanajidai kupokea uamsho? Kama kweli Waarabu wanajinasibu kuwa walikuwa wanasayansi wakubwa duniani, kwa nini leo hii ni tofauti? Kwanini Jihad? Kwanini Crusades? Kwanini Waarabu hawasaidiani, je huo ndio Uislamu?.. kwa nini “kwa nini” ni nyingi? Ni maswali unayoweza kujiuliza na wala sio dhambi kujiuliza haya maswali, tafuta majibu yake.

Baada ya kujiuliza maswali yote hayo swali moja la msingi linahitaji majibu ya kweli. “Je sisi tumetoka wapi?” Mwaka 65 KK, jeshi la Warumi chini ya Jenerali Pompey waliuteka mji wa Yerusalemu. Mnamo mwaka 70 BK, (Luke 21:24) Jenerali Vespasian na mwanae wa kiume Tito waliumaliza kabisa uwepo wa taifa la Kiyahudi, kwa mauaji makubwa mno kupata kutokea kwa wakati ule, mashambulio yalikuwa makali na yaliwadhuru watu wengi sana. Watu waliobaki walifanyiwa mauaji makubwa sana. Kutoka kipindi cha Pompey hadi Julius inakadiriwa kuwa zaidi ya Wayahudi 1,000,000 walikimbia Yerusalemu kwenda Afrika (Luke 21:12), walikimbia unyanyasaji, utesaji na kufanywa watumwa na Warumi. Biashara ya watumwa ilikuwa imejaa Waafrika (Watu Weusi), ukisoma kitabu cha, Windsor R. From Babylon to Timbuktu, pg. 84. Rudolph Windsor amefuatilia historia ya Waebrania weusi, kuanzia mwaka 70 BK, akiangalia asili yao kuanzia Babeli tokea kwa Abraham, kuzaliwa kwao hadi walipokuwa wakiishi Kaanani. Alijikita pia kuangalia historia ya Waebrania Weusi wwa Ethiopia, Misri, akitoa ushahidi pia wa Tabiban Kamant na Wayahudi Wasambara wa Tanzania ambao kwa sasa wanajulikana kama “Falasians” ambao wapo huko Ethiopia pia. Amejikita pia kuangalia historia ya Wayahudi walioko huko Madagaskar. Kama ambavyo nilikwisha kueleza hapo awali kwamba Waafrika ndio Waisraeli wanaozungumziwa kwenye biblia takatifu na wanazuoni wa biblia wanajua hilo kwa uwazi kabisa (Fanya kutembelea Makumbusho ya Mapango ya Amboni na makumbusho ya Mapango ya huko Kondoa)..

Endelea...

0 maoni :

Popular Post

Subscribe to Newsletter

We'll never share your Email address.
© 2015 Tanzania Conservative. Designed by Conservative. Powered by Blogger.