Kufichika kwa baadhi ya historia
Ukifuatilia historia ya Tanganyika ni ngumu sana kuona mahali imetajwa kwa
jina hilo la Tanganyika. Achana na historia baada ya Wazungu kugawana eneo hili
na kulifanya koloni lao; nazungumzia historia yake kwa miaka ya nyuma kabisa ya
karne ya kumi na nane. Utagundua kuwa katika vitabu vya kihistoria wana sema
juu ya “Great Lakes Nation” au Taifa
la Maziwa Makuu; wengine wanaandika Taifa la Wabantu (Bantus Nation) ambao wametokea kutokea Ethiopia wengine wanasema
kutokea Kongo ambapo kulikuwa na mababu wa Punt
wa huko Misri. W.E.B. Du Bois (1915),
“The Negroes” anaandika na kusema
kuwa Wabantu (Nilotic Negroes) walifanikiwa kupigana na kuwasukuma “Bushmen” au
Hottentot (type of Negores) huko Kusini na Magharibi mwa Afrika kutoka eneo la
maziwa makuu (Afrika Mashariki na Kongo) anasema kuwa Negroes walikuwa huko Ufa
wa Nile (Nile valley) ambapo uzao wa
pili ulichanganyika na kuwa na damu ya
Semetic (Waebrania, Wayahudi au Waisraeli) anadai kuwa kwa miaka zaidi ya 5000
KK, machotara (mulatto) wa Kimisri na Wazungu walikuwepo na walikuwa
wakiishi
huko Bonde la Mto Nile kwenye maporomoko ya kwanza, na Negroes walikuwa
wakiishi kwenye maporomoko ya pili ambao anadai kuwa damu ya Uisraeli (semitic
blood) ilikuwa imechanganyika zaidi au kidogo. Anasema kuwa jamii hii ndiyo
sasa ni wazawa wa Somali, Gala, Bishari, na Beja za sasa na kusambaza damu hii
huku Red Sea na Uarabuni. Anasema kuwa biashara na kuhamahama kunaifanya
historia ya Wabantu wa Maziwa Makuu kuwa ngumu kuelezeka na kuielewa. Anasema kuwa kuna unasibu mkubwa mitatu,
kwanza ni kwamba asili ya Wabantu wa maziwa makuu ni Misri,kama waamiaji
wakutokea Kaskazini mwa utawala wa mwanzo wa Misri waliokuja kushika na
kutawala soko la kusini ya Misri, pili ni Waebrania, Wayahudi, Waisraeli (Semitic) waliokuwa wameathiriwa na
Uarabu na Uajemi; tatu, ni Wabantu (yeye amesema Negros) kutoka Magharibi na
Afika ya Kati, (Bois, (1915), The Negroes, uk. 97).
Upatikanaji wa teknolojia kati ya Wabantu katika kilimo cha umwagiliaji,
uchimbaji wa madini, ufugaji uliwasaidia kuweza kufanya biashara sehemu
mbalimbali duniani. Wabantu walifanya biashara hadi Asia ya mbali. Biashara ya
Dhahabu, kopa na silva iliwapa nguvu na inasemekana pia ndio moja ya dhahabu
zilizokuwepo huko Ophir. Jambo hili
lilifanya kujengwa kwa taifa huko Benomotapa, Zimbambwe ya sasa. Ambapo kuta
zake imegundulika kuwa zilikuwa zimejengwa kwa ustadi mkubwa sana . Jengo
lilikuwa ni ngome iliyokuwa na sehemu ya kuweka wanyama, karakana, sehemu za
kulala, na uwanja kubwa. Kuna masalia mbalimbali ya kale yaliyopatikana huko
Zambezi na maeneo mengine, sanaa ambazo ni nzuri za kuvutia.
Mwaka 1590, huko ambako kwa sasa ni nchi ya Msumbiji kulikuwa na usambaaji
mkubwa watu usiokuwa na idadi wakitokea huko Mwanamutapa (Monomotapa) hawakuacha kitu chochota kusalia. Bois katika kitabu chake aliwaita hawa wapagani. Imeelezwa juu ya
ujio wa watu waliokuwa wanaitwa Zimbas;
watu wanaotisha ambao hawajawahi kuonekana waliokimbia nchi yao huko na kuja
waliokuwa wamepita sehemu kubwa ya Ethiopia wakiwa wanaua kila kitu kilichopo,
kama ambavyo miaka mia nne Wazulu walivyojipanga. Mwaka 1602 watu kutokea ndani
kabisa, waliokuwa wanaitwa Cabires/Canibbals
“Wala watu” waliingia kwenye Ufalme wa Mwanamutapa, na Mfalme aliyekuwa
anatawala pale alikuwa dhaifu na ufalme wake ukaanguka na kutawanyika mpaka
sasa kuwepo kwa Kaffir-Zulu.
Mwandishi wa Kiarabu aliyeita Macuodi, alifika iliyoitwa
Bahari ya Hindi kwatika Afrika a mashariki na kukuta vitu vyenye asili ya
Uarabuni ila hakukuta makazi yoyote yaa Waarabu isipokuwa wakazi wa huko
waliitwa Wabantu au kama wanavyojiita wenyewe Wazenji, wakiwa wametwaa nchi
kusini mwa Sofala na walikuwa wamepakana na Bushmen (Bushmen ni wakina nani
hasa?) kiongozi wao alikuwa ana cheo kinachoitwa “Waklimi”( The Negros, pg.
50). Na nchi hiyo ilikuwa ikizalisha dhahabu kwa wingi sana huku ngozi ya Chui
ikitumika kama vazi. Mwaka 1330 Ibn Batuta alikwenda Kilwa ambayo ilikuwa
kiungo kizurisana cha kibiashara Afrika mashariki ambapo Kilwa yenyewe ilikuwa
na misikiti zaidi ya 300, Batuta alijizolea ushindi dhidi ya Wazenji/Wabantu.
Baada ya kutekwa kwa Kilwa, Sofala ilisimama kutokea Mogadishu. Hata hivyo Kilwa
ilikuwa kama kitovu kikuu cha taifa zingine ikiwemo Zanzibar, Msumbiji, na
mamlaka zingine (Tanganyika haijatajwa kwa jina!, kwa nini?) Wakati wa utawala
wa aliyekuwa Mfalme wa 43 wa Kilwa baada ya kuutwaa mji, aliyeitwa Abraham
alikuwa akifanya biashara na Watu wa mamlaka ya bara ambao walikuwa mjumuiko wa
kabila nyingi walioitwa Wabantu.
0 maoni :