Jumapili, 30 Julai 2017

JE WEWE NI NANI?-1

Tanzania Conservatives     Julai 30, 2017     No comments


Utangulizi


Kabla ya kufanya uchambuzi huu wa wazi na kujikita ndani kabisa kuna mambo ya msingi ya kujiuliza kabla ya kuchimba Zaidi, kwanza fahamu kwamba kutafuta ukweli juu ya jamii yako au dini yako sio dhambi ni moja kati ya njia ya kujitambua na kumwamini Mungu wako wa Kweli. Kama unawasiwasi sana naomba ujikaze na uwe tayari kujibu maswali haya.
Watu Weusi wakifanya kazi kama watumwa Misri


  • Unajua nini juu ya jamii yako kama mwafrika?
  • Kabla ya biashara ya utumwa wazazi wako walikuwa wa asili hiyo uliyoko?
  • Je Katika jamii yako kuna watu ambao walikuwa wanafanya kazi za ubunifu kama kutengeneza zana za Kilimo, kufua chuma nk?
  • Je jamii uliyoko unajua nini juu ya mababu wako?
  • Je unafahamu kizazi cha nne nyuma ya hiki ulichopo?
  • Je Mababu zako walikuwa wanamwabudu Mungu yupi kabla ya wakoloni?
  • Je majina ya asili yako kwanini huyatumii kama unayatumia kwanini una jina la kizungu?
  • Je kwanini katika historia tunayosoma mashuleni inazungumzia kuanzia karne ya 16 kwa Afrika wote na karne ya 18 kwa Tanganyika?
  • Je Katika biblia tumezungumzwa wapi Katika kizazi cha Nuhu na watoto wa Yakobo?
  • Je tuna vinasaba na Waisraeli?
  • Je ipi ilikuwa Misri ya mwanzo wakati ule wa Abrahamu hadi Mussa?
  • Kwanini Waisraeli waliuzwa kama watumwa?
  • Kwanini Waafrika waliuzwa kama watumwa?
  • Je kama kweli tuna mahusiano na Black americans/Negroes kwanini waliitwa Negros?
  • Je Negros wko Marekani tu?
  • Kwanini watanzania wengi wanafanana na wanigeria na waghana?
  • Kwanini vita ya majimaji ili chukuwa muda mrefu?
  • Je ni kweli kwamba Mkwawa alijiua?
  • Kwanini waafrika waliwauza waafrika wenzao kama watumwa?
  • Kwanini historia inasema kuwa tumetokea kutoka magharibi mwa Afrika?
  • Kwanini historia inafichwa?

Kwa maswali hayo baadhi unaweza kugundua kuwa moja kati ya sii kubwa zinazofichwa ni juu ya historia ya mtu mweusi (Waafrika). Tukutane kwenye andiko la pili. Inabidi kuandika kwa kifupi ili tusichoke kujua ukwe huu ukubwa ambao naenda kukuandikia.

Endelea sehemu ya pili

0 maoni :

Popular Post

Subscribe to Newsletter

We'll never share your Email address.
© 2015 Tanzania Conservative. Designed by Conservative. Powered by Blogger.