Wewe kama mwafrika
Ham akiwa na nduguze(Watoto wa Nuhu) |
Utajiuliza kuwa kwanini Katika historia ya
mwafrika tumejikita sana kuanzia biashara ya utumwa, biashara ya kupitia jangwa
la Sahara nk. Utajua kuwa kuna siri kubwa inafichwa nyuma ya pazia. Tuchimbe kuanzia
enzi ya Nuhu, mototo wake wa nane aliyeitwa “Ham”ambaye kwa mujibu wa “Book
of Genesis” ndiye baba wa Watu Weusi. Ham
alikuwa na watoto, kwa majina walikuwa wanaitwa:
- Kushi (Utawala wa Kushi, Sudani ya kale), ambaye alikuwa kaka wa Kanani
- Kanani(Canaan) wa Kanani(ndio Kanani ile tunayoimba kutoka misri kwenda Kanani),
- Mizraimu (wa Misri) ambaye ndiye Waebrania na Aramaic na
- Phut( wa Libya) ambapo ukisoma kwenye kitabu cha (Nahumu 3:1-18) kinaeleza juu ya kujengwa kwa taifa la Libya.
Swali ni kwanini Katika
kamusi ya biblia ya Zendervan wamewaacha Negroes Wamarekani, je sio weusi?
Jua kwamba kulikuwa na Waafrika wa asili Katika
Afrika(Native Africans) na kuna Waafrika ambao ni Wayahudi(Black Jews) mfano kabila
la Igbo. Hawa ndio wale ambao pia wamesambaa na kuenea Katika Afrika ya
Mashariki pia. Waingereza walikuwa moja kati ya wanunuaji wakubwa wa watumwa
hadi pale walipo acha biashara hii mwaka 1807, na biashara hiyo kushika kasi
kwa Wareno na Wahispania kuwa vinara wa biashara hiyo na mateka wengi waliouzwa
kama watumwa ni watu wa kabila la Igbo
(Prof. Eltis, D. na Prof. Richardson, D., “Atlas of transatlantic
slave trade” pg. 127). Ndio hao ambao pia wamepelekwa Amerika na kupewa jina la Negros. Na hao
wote ni wana wa Israeli pia.
Biashara ya Utumwa ya Waisraeli Weusi |
Ukisoma (Yoeli 3:4 “Naam, nanyi ni kitu
gani kwangu, enyi Tairo na Sidoni, nan chi zote za Filisti? Je mtanirudishia
malipo? Au mtanitenda neno lolote? Upesi na kwa haraka nitarudishia malipo yenu
juu ya vichwa vyenu wenyewe.”) Tairo na Sidoni hizi ni nchi za asili ya Lebanoni
ambazo huko nyuma inasemekana zilikuwa zinakaliwa na Watu weusi wa Kiyahudi. Ambapo
ukiendelea mbele (Yoeli 3:5) wizi na uporaji uliotokea kwa Waisraeli wa silva na
dhahabu pamoja na vitu vizuri vya waisraeli ikiwa pamoja na kuuzwa kwa watoto
wa Yuda(Wayahudi Weusi) na watoto wa
Yerusalemu kwa Wayunani(Greece). Ili
waondolewe nakutupwa mali ya mipaka yao. Amapo hapo kwenye (Yoeli 3:8) Mungu anasema juu y adhabu itakayowapata waliowavamia Wayaudi
weusi na Wayerusalemu, kwamba watatawaliwa na watu wa mbali kabisa watu wa
Sheba(Waethipia). Na kweli Wataliano
walipigwa na Waethipia wakati walipotaka kuwatawala.
Je Misri ya leo kwanini si
waafrika kama unavyosema nani Waarabu na Mashariki ya kati waliopo ni Waarabu
na Wazungu? Jibu ni jepesi kwamba hadi sasa Waisraeli hawajarudi Katika nchi yao,
kwani maandiko yanasema kuwa watakaporudi wana wa mji hakutakuwa na machafuko. Angalia
yanayoendelea. Hao ni akina nani? Hao ni warumi wanao jidai kuwa Waisraeli.
Utagundua kuwa jamii ya watu wa Ngoni ni
wahanga wa machafuko yale. Swali la msingi haaa ni kwamba kwanini baada ya
uvamizi wa Wazungu (Wadachi kusini mwa afrika) wahamiaji walizidi kwa kasi
kubwa kwa miaka hiyo ya 16? Historia inatuambia kuwa watu wa mashariki ya
Afrika walitoka kutoka Magharibi mwa Afrika! Ulishajiuliza kwa nini kutoka
Magharibi mwa afrika? Turudi Katika maandiko matakatifu juu ya eneo ambalo
Wamisri waliwapa Waisraeli kuishi; kusini mwa Misri huko Waisraeli waliendelea
kuenzi tamaduni zao.
Sisi ni akina nani? Majibu ya mwanzo ya swali
hili embu tuangalie kwenye biblia (Wim 1:5), “Mimi ni mweusi-mweusi, lakini ninao mzuri, enyi binti za Yerusalemu, mfano
wa hema za kedari, kama mapazia yake Sulemani.” Mfalme Sulemani alikuwa mtu
mweusi. Sisi ni Waisraeli!
0 maoni :