Sikukuu ya Kwanzaa iliasisiwa na aliyekuwa Profesa na mwenyekiti wa stadi za mtu mweusi, Dr Maulana Karenga wa chuo cha California State university mnamo mwaka 1966. Baada ya machafuko na migomo ya watu weusi mwaka 1966 huko Los Angeles, Dr Karenga Alita futa njia nzuri ya kuwarejesha pamoja watu weusi Marekani.
Alianza kwa kufanya tafiti kufahamu mazao ya mwanzo ya Waafrika na sherehe zake. Aliunganisha dhana ya sherehe mbalimbali za mavuno kutoka kabila la Ashanti na Zulu wa Afrika ya Kusini, alifanya hivi kujenga misingi ya siku ya Kwanzaa.
Neno Kwanzaa limechipuka kutoka kwenye dhana ya "matunda ya kwanza" kwa lugha ya Kiswahili. Ambapo familia na kabila mbalimbali zinasherekea kwa nyimbo na namna yao ya asili kwa ngoma, kuimba, kueleza hadithi na kwa kufanya karamu ya vyakula.

Katika kila sik, kuanzia tarehe 26/12 kila mwaka kwa muda wa siku saba mshumaa unawashwa katika kinara, ambapo mishumaa hii ina rangi tofauti kila rangi ikiwa na maana yake. Anayewasha mshumaa ni mtoto na na hapo mjadala wa kanuni moja wapo ya kanuni saba hujadiliwa katika siku yake. Kanuni hizi huitwa "nguzo saba" ambapo kwa msingi wake hujali na kuthamini tamaduni ya mtu mweusi.
Vilevile kuna alama za Kwanzaa ambazo zipo saba kilele cha Kwanzaa huwa tarehe 01/01 na siku hii huwa siku ya KARAMU. Siku hii huitwa "karamu"
.
Nguzo saba za Kwanzaa

1. Umoja
Hii huwa tarehe 26/12 ya kila mwaka ambapo katika umoja jamii inakuwa katika hali ya upamoja katika umoja. Siku hii mafundisho ya masuala ya umoja hujadiliwa.

2. Kujichagulia
Hapa ni kueleza na kujipambanua wewe ni nani na kipi unakihitaji.

3. Ujima
Kuijenga jamii yetu kwa pamoja na kufanya matatizo ya ndugu zetu kama yetu na kusaidiana kuyatatua.

4. Ujamaa/uchumi wa ushirika
Kujenga na kuendesha maghala, maduka, biashara mbalimbali kwa ushirika kujenga kipato cha faida kwa maendeleo yetu.

5. Nia
Uthubutu wa kuwa tayari kujenga na kuendeleza jamii ili kudumisha utu na ukuu wa tamaduni zetu.

6. Kuumba
Kufanya kwa vyovyote vile katika ubunifu kwa namna inayofaa ili jamii inayotuzunguka iweze kudumu na kupendeza na kwa manufaa zaidi kuliko tulivyo irithi.

7. Imani
Kuwa na matumaini na watu wetu, wazazi, walimu, viongozi kuwa na tumaini katika kweli na ushindi wa mapambano yetu